Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde amekabidhi Gari Moja ya kubebea wagonjwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Jijini Dodoma.

Akizungumza katika makabidhiano hayo hii leo Mei 9, 2024 Mavunde amesema gari hiyo ina uwezo wa kumfuata mgonjwa katika mazingira yoyote.

Amesema, “tumebaini kuwa kuna wagonjwa wapo wilayani ambapo tunalazimika kuwafata huko wilayani, na hii gari inauwezo wa kwenda Kumfata mgonjwa mahali popote zaidii.”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Alphonce chandika ameshukuru kwa kupatiwa gari hilo na kusema kwasasa wana uwezo wa kuwabeba wagonjwa mahali na Wilaya yoyote.

“Katika hospitali hii tuna jumla ya magari Matatu ya kubebea wagonjwa, mengine mawili yalikabidhiwa miezi mitatu nyuma mwaka huu,” amesema Dkt. Chandika.

Kerveillant aomba kazi Simba SC
Kitaeleweka baada ya EURO 2024