Kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara ya Maji inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi 1,200,001,000, kutokana na vyanzo vya mauzo ya Nyaraka za Zabuni, Leseni kwa Kampuni za utafiti na uchimbaji wa Visima vya Maji, Tozo mbalimbali kwa wateja wanaopata huduma ya Maabara za Ubora wa Maji na Vibali vya Matumizi ya Maji katika Mabonde.

Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo Mei 9, 2024 na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati akitoa taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na mazingira kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na maoni ya kamati kuhusu makadirio ya ya wizara.

Amesema, “malengo na vipaumbele vilivyoainishwa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, vinaendana na majukumu ya Msingi ya Wizara ya Maji, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, na awamu ya nne ya mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano mwaka 2021/22 – 2025/26, ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na ahadi mbalimbali za Viongozi wa Kitaifa.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Aweso ameongeza kuwa, “Wizara inaendelea kutekeleza Miradi ya Maji kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mujibu wa eera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002, sheria ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009 na maboresho yake ya mwaka 2022,Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019 pamoja na Kanuni zinazoelekeza utekelezaji wa Sheria hizo.”

Hata hivyo amesema uchambuzi wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji ulifanyika kwa kuzingatia kazi zilizopangwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kuimarisha Usimamizi, Uendelezaji, Uhifadhi na Utunzaji wa vyanzo vya Maji, kuimarisha huduma ya usimamizi wa ubora wa maji nchini, kuboresha huduma ya Maji katika maeneo ya Mijini, kuboresha huduma ya Maji Vijijini na kuimarisha uwezo wa kitaasisi.

Idris Sultan azua gumzo Afrika kusini, uzinduzi Show mpya ya Netflix
Ngoma awapa masharti viongozi Simba SC