Jaji Mkuu wa Kenya, Martha Koome ametahadharisha Taifa kuingia katika mgogoro wa kikatiba, iwapo viongozi wakuu nchini wataendelea kupuuza maagizo yanatolewa na idara ya Mahakama.

Jaji Koome ameyabainisha hayo na kusema wameandika barua kwa Ofisi ya Rais, William Ruto kuomba kufanya naye kikao kubaini ni majaji gani wanakwenda kinyume na utendaji wa kazi, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Wakati hayo yakijiri, tayari Baraza la Mawaziri limeidhinisha utekelezwaji wa mfumo wa akaunti moja ya fedha za Serikali (TSA), itakayotumika na Serikali kuu na Kaunti.

Akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri, Rais William Ruto alisisitiza umuhimu wa TSA katika kurahisisha huduma za Benki za Serikali, kuunda sehemu moja ya kuingia fedha zinazolipwa kwa huduma mbalimbali na uwazi katika usimamizi wa fedha.

Makala: Shujaa Kunta Kinte na dhana ya ukombozi
Wazazi jengeni ukaribu na Watoto - Mutabihirwa