Miili tano imeopolewa katika mto Kwa Muswii uliopo eneo la Kasikeu huko Sultan Hamud kaunti ya Makueni Nchini Kenya, baada ya Lori lililokua limebeba zaidi ya watu 10 kusombwa na maji ya mafuriko.

Tukio hilo, limetokea mchana wa Aprili 26, 2024 ambapo wapiga mbizi walifanya juhudi za ziada ili kuokoa watu waliosombwa na maji ambayo yalikuwa na kasi na kufanikiwa kuwanusuru watu 11 wakiwa hai.

Lori hilo, lililokua limebeba zaidi ya watu 10 lilisombwa na maji ya mafuriko, katika eneo hilo wakati likijaribu kuvuka eneo ambalo halikuwa salama na lililokuwa likipitisha maji kwa kasi.

Hata hivyo, licha ya mvua kuendelea kuleta madhara Waathiriwa wa mafuriko ambao wamekuwa wakikaidi agizo la kuhama maeneo hatari kaunti ya Kilifi, sasa wanatakiwa kuhama maeneo hayo la sivyo wataondolewa kwa nguvu ili kuepuka maafa.

Mkurugenzi mkuu katika Ofisi ya Mbunge wa Malindi, Juma Kilo na Mratibu wa mipango katika ofisi hiyo, Dickson Chilango wamesisitiza kuwa ipo haja ya watu wote walio sehemu hatari kuondoka kwa haraka.

TUCTA: Rais Samia kulizindua Mfanyakazi Tanzania
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 27, 2024