Bertina Mangosongo.

Ili kuwawezesha Vijana kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya Kilimo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako amehimiza ushirikiano baina ya ofisi hiyo na Wizara ya Kilimo.

Akiongea katika hafla ya mapokezi ya vijana 268 wanufaika wa programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT), katika Shamba la pamoja la Chinangali II Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Prof. Ndalichako amesema na serikali imeanzisha programu hiyo, ili kupunguza tatizo la ajira, hivyo wakiwezeshwa kufanya kilimo biashara wataweza kujiajiri, kuajiri wenzao na kuongeza mchango wa sekta ya kilimo na pato la Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Vijana hao wa BBT wamekabidhiwa vifaa wezeshi vya kilimo pamoja na mashamba na wataanza na kilimo cha alizeti katika eneo hilo la Chinangali II.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ameeleza kuwa programu hiyo ya Jenga Kesho Iliyo Bora itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa chakula nchini.

MALIMWENGU: Dhihaka yenye kweli ndani yake
Zaidi ya 500 wapata Matibabu Magonjwa ya Moyo