Lydia Mollel – Morogoro.

Harakati za kutengeneza na kuboresha miundo mbinu ya Barabara, ili kuwawesha Wananchi kufanya shughuli zao kwa uharaka zaidi imegeuka kero kwa Wananchi Mtaa wa Sadani na Mtaa wa Mfunguakinywa Kata ya Mwembesongo Mkoani Morogoro, mara baada  ya kuharibiwa kwa miundombinu inayopitisha majitaka na maji safi katika eneo hilo kufuatia mradi Wa ujenzi wa Barabara inayopita katika eneo hilo kuelekea Msamvu.

Wakizungumza na Dar24 Media, Wananchi hao wamesema uwepo wa maji hayo katika eneo hilo linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu lakini pia changamoto kubwa ni ukosefu wa maji Safi na salama, huku Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sadani akisema ni miezi miwili sasa tangu Barabara hiyo ichimbwe, ambapo imesababisha uchafuzi wa mazingira pamoja ukosefu wa huduma ya maji Safi na salama.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Mohamed Mwanda, amesema tayari  wamepewa gharama za matengezo ya miundombinu iliyoharibika na wamemuelekeza Mkadarasi kuzilipa ili miundombinu hiyo ianze kurekebishwa.

Licha ya uharibifu ya miundombinu ya vyanzo vya maji uliojitokeza, pia kumekuwa na desturi ya utiririshaji maji taka maeneo mbalimbali katika kipindi cha Mvua, suala ambalo husababisha uchafuzi wa Mazingira katika vyanzo vya Maji na kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko.

AFCON 2023: Avram Grant achimba mkwara mzito
AFCON 2023: Stars ni KUSUKA ama KUNYOA