Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amezindua programu ya Kopa Ngo’mbe Lipa Maziwa, yenye lengo la kuwainua kiuchumi Vijana na Wanawake Nchini.

Ulega amezindua programu hiyo katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe 300 kwa Kampuni ya Kahama Fresh, ambao watakopeshwa kwa wanufaika hao, ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia uzalishaji wa maziwa.

Alisema, “Programu hii ya Kopa Ngómbe Lipa Maziwa imekuja kwa wakati muafaka na itaongeza kasi ya juhudi za Serikali kuleta mabadiliko ya kisekta kupitia Wizara. Hivyo, nawahimiza wafugaji kuwatunza ng’ombe watakaopewa ili kupata tija inayotarajiwa na kuhakikisha wanafuga kisasa.”

Katika uzinduzi huo, Waziri Ulega alikabidhi Ng’ombe 300 kwa awamu ya kwanza kati ya ngombe 600 ambao watawakopeshwa kwa Wafugaji, ili waweze kuzalisha Maziwa na kupeleka malighali kwenye kiwanda cha Kahama Fresh.

Programu ya Kopa Ng’ombe Lipa Maziwa inaendeshwa na kampuni ya Kahama Fresh kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Shirika la Heifer International na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

RC Sendiga ataka ufanisi wa usambazaji Maji
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 24, 2024