Klabu ya Manchester United imekataa mpango wa Inter Milan wa kumsajili Aaron Wan-Bissaka kwa makubaliano ya kubadilishana na beki wao wa pembeni Denzel Dumfries.
Beki wa kulia Wan-Bissaka mwenye umri wa miaka 26, ameanza kwenye mechi kumi chini ya Kocha Erik ten Hag msimu huu, licha ya kukosa kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na tatizo la misuli ya paja, na anaonekana kama kiungo wa thamani wa kikosi hicho.
Mkataba wake ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini United sasa wamenza mazungumzo ya kumuongeza na kumfanya abaki Old Trafford hadi 2025.
Uamuzi wa Inter kumtoa Dumfries, ambaye amecheza mara 18 msimu huu, bado ni mshutuko kwa kuwa staa huyo mwenye miaka 27, ni mmoja wa walinzi bora wa kulia kwenye Serie A.
Mkataba wake na Nerazzurri utamalizika Juni 2025 na bado anaweza kuondoka msimu wa joto kwa kuwa kuna mvutano wa mkataba mpya Dumfries anataka mshahara wa pauni 80,000 kwa wiki, lakini Inter wanatoa pauni 35,000 tu kwa wiki.