Inaelezwa kuwa klabu ya Raja Casablanca ya Morocco ipo katika mpango wa kumsajili aliyekuwa Mshambuliaji wa Simba SC, Jean Baleke ambaye ni moja kati ya wachezaji walioachwa na timu hiyo kupitia dirisha dogo.

Baleke ni moja kati ya wachezaji walioachwa na Simba SC kupitia dirisha dogo sawa na Moses Phiri ambaye ametolewa kwa mkopo katika klabu ya Power Dynamos ya Zambia.

Taarifa kutoka katika uongozi wa unaomsimamia mchezaji huyo umeweka wazi kuwa na mazungumzo na uongozi wa Raja Casablanca ambao umeonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo ajiunge na timu yao.

“Baleke kwa sasa anawindwa sana baada ya kuondoka Simba SC, timu kama Raja Casablanca inaongoza kwa sasa katika mbio za kumsajili lakini pia AS Vita nao ni moja kati ya timu ambayo inataka kujaribu kumsajili.

“Baleke ni mshambuliaji mzuri sana ambaye naamini anatakiwa kupata timu kubwa na nzuri na sahihi kwake, ni suala la muda tu utamuona akiwa na timu tena kubwa, maisha ya mpira ndio yapo hivyo na hakuna kuangalia nyuma kwa sasa.” amesema Faustino Mkandila wakala wa mchezaji huyo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 26, 2024
Man Utd yaishtukia Inter Milan