Kufuatia mvua inayoendelea kunyesha Mkoani Morogoro, imesababisha mafuriko yaliyopelekea barabara za katikati ya mji kutopitika kutokana mitaro kujaa maji.
Wakizungumza na Dar24 Media, Wananchi waliokuwepo eneo hilo wameelezea adha wanazozipata kutokana na maafuriko hayo lakini pia kupelekea maduka ya wafanya biashara kujaa maji.
Wamesema, Mvua hiyo wainakadiriwa kunyesha kwa zaidi ya saa moja na kupelekea mawasiliano ya barabara kukatika lakini pia shughuli za kijamii kukwama.