Wazee wa Kijiji cha Utengule kilichopo Kata ya Kifanya, Tarafa ya Igominyi Wilayani Njombe, wameaswa kuacha tabia ya kunyanyasa wenza wao kwani hali huleta manyanyaso na hata kupelekea mauaji au kusambaratika kwa familia.

Rai hiyo, imetolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Kifanya, Mkaguzi Magreth Flowin Mbawa ambaye amesema matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakitokana na kwa Wanaume kuwanyanyasa Wanawake.

Amesema, hali hiyo hupelekea mauaji na kuacha familia zikiangaika kitu ambacho kinapaswa kukemewa na kwamba Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vya aina hiyo na sheria itachukua mkondo wake.

Aidha, Magreth pia amewataka Wazee hao kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapomkamata mtuhumiwa, na badala yake watoe taarifa kwenye mamlaka zinazohusika ili hatua zichukuliwe huku akiwataka pia kuendelea kutoa taarifa za uhalifu bila kumuonea mtu muhali.

Dhamana ni haki ya yeyote, hainunuliwi - Polisi
Uzalishaji Mbolea: GST, TFRA, TFC wasaini makubaliano