Lydia Mollel – Morogoro. 

Vijana Mkoani Morogoro wametakiwa kutambua Elimu waliyonayo isiwafunge na kuona yenyewe ndio itakuwa chanzo cha mafanikio yao katika maisha  badala yake kutumia elimu waliyonayo hili  ziwasaidie kufanikiwa katika maisha.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro ambaye pia ni mkurugenzi wa Ruby International Limited Salim Alaudin Hasham katika kongamani la vijana wa vyuo vikuu na vyakati University ladies and Gentlemen conference iliyoandaliwa na Taasis ya Ladies Talk Tanzania katika ukumbi wa Chuo Kikuu Sua Mazimbu Campus Mkoani  Morogoro .

Amesema, changamoto kwenye maisha ni zawadi ambayo inamfanya mtu kuumiza akili zaidi ili apate suluhisho la tatizo lakini pia uthubutu kwenye maisha kwani kuanguka sio sababu ya mtu kufeli kwenye maisha.

“Nilazima huweke mazingira ya kuhifadhi pesa na kuilinda ukifanya mistake kinachofwata huwezi kurudia hiyo mistake ambayo humefanya” Amesema Salim Alaudin

Mbunge huyo, ametoa shilingi millioni moja kwa mfanyabiashara mdogo hili kumuweza kukuza biashara yake hanayofanya kwani amekuwa na uthubutu wa kufanya jambo

Naye Faudthia Ally mfanyabiashara wa Rangi aliyepewa mtaji amemshukuru mbunge huyo na kuwataka vijana kuchangamkia fursa yoyote wanayoipata kwani itawasaidia kufanikisha ndoto yao na kuwa msaada kwa wengine.

Hata hivyo, kongamano hiyo iliudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkurugenzi wa masoko BBT ,wafanyabiashara pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu na vyakati vilivyopo mkoani Morogoro.

Wabakaji wakalia kuti kavu Kagera
Upendo, furaha vyatawala 'Polisi Family Day' Moro