Johansen Buberwa – Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajath Fatma Mwassa ametangaza vita na watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji kwa kwa watoto wadogo na kuwaagiza Wakuu wa Wilaya zote ndani ya Mkoa huo, kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza wakati wa kufungua wiki ya sheria Mkoani Kagera katika viwanja vya Mahakama ya Kanda ya Bukoba January 28 mwaka 2024 Mwasa amesema miongoni mwa changamoto zinazo ukabili Mkoa huo ni pamoja na kesi nyingi za ubakaji ambazo zimekuwa zikipewa dhamana na wengine kufikia hatua ya kuharibu ushahidi.
Amesema, “nipo tayari kutumia rasilimali zote tulizonazo kwenye Mkoa watu wa Kagera kwa kuhakikisha tunaweka mawakili wazuri ili kushinda kesi za ubakaji, natangaza vita uwe na hela,uwemfanyabiashara mkubwa au mchawi tutalala na wewe bega kwa bega hatuko tayari kuona ubakaji unashamili katika huu Mkoa tutawashughulikia kikamilifu.”
Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kanda ya Bukoba, Imakulata Banzi amesema katika wamefanikiwa kutoa elimu ya sheria ikiwemo ndoa na talaka, utatuzi wa migogoro ya ardhi, kazi, madai, jinai, mtoto na makosa ya kujamiana.
Mengine ni makosa ya mauaji pamoja na sheria za Rushwa na uhujumu uchumi kwa taasisi na zaidi ya shule za Msingi na Sekondari 40 mikusanyiko ya watu ikiwemo stendi na masoko, maingilio na pembezoni mwa ziwa victoria katika mialo na vyombo mbalimbali vya habari na jamii kwa ujumla.
Awali, Afisa ustawi wa jamii Mkoani Kagera Rebecca Gwambasa alipo hojiwa na vyombo vya habari amesma kwa kipindi cha mwaka 2023 kuanzia Januari hadi septemba wamepokea mashauri ya ubakaji na ulawiti kwa watoto 102 na yalipelekwa Mahakamani na kati ya hiyo zimeshatolewa hukumu.