Kocha kutoka nchini Ujerumani Jurgen Kohler ametuma maombi ya kuwania nafasi ya Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana ‘Black Stars’.

Kohler amewasilisha maombi yake mbele ya kamati maalum inayoundwa na wajumbe watano, ambayo bado inayoendelea kupokea maombi ya makocha mbalimbali walionesha nia ya kutaka kukinoa kikosi cha Ghana, huku mwisho wa kupokea mambo hayo ukitajwa kuwa Februari 2, 2024.

Kamati hiyo inaongozwa na Makamu wa Rais wa GFA Mark Addo huku mwanasheria Ace Ankomah akiwa makamu wake.

Vyombo vya habari vya Ghana vimeeleza kuwa Kohler anapewa nafasi kuwa ya kukabidhiwa jukumu la kuwa Kocha Mkuu wa Black Stars, licha ya mchakato wa kupokea maombi kuendelea kwa sasa.

Kohler, ambaye ana Leseni ya UEFA Pro, alihudumu mara ya mwisho kama mkufunzi wa muda katika FC Viktoria Koln mnamo 2019. Licha ya kukosa uzoefu mkubwa wa ukufunzi wa kiwango cha juu, maombi yake yamekuwa gumzo nchini Ghana.

Kocha huyo amewahi kukinoa kikosi cha Ujerumani chini ya miaka 21, pia amewahi kuwa mkurugenzi wa Soka katika Bayern Leverkusen kuanzia Machi 2003 hadi Juni 2004.

Aliiongoza MSV Duisburg, na pia alikuwa mkurugenzi wa soka katika timu ya daraja la tatu ya Ujerumani vfR Aalen.

Akiwa mchezaji Kohler aliwahi kushinda Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani na Ligi ya Mabingwa ya UEFA akiwa na Borussia Dortmund.

CAF yambananisha Osimhen Ivory Coast
Chasambi apewa mbinu za kuishi Simba SC