Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limemkamata mtu mmoja Dayano Swaum Chowo, (49), Mkazi wa Naholo akiwa na Fuvu lidhaniwalo kuwa la binadamu na vipande vitatu vya ngozi wanyama pori akiwa amevihifadhi ndani ya begi dogo la mgongoni na kuvificha katika nyumba anayoishi.
Mtu huyo, alikamatwa Januari 7, 2024 wakati wa operesheni, misako na doria inayotekelezwa katika mbalimbali maeneo ya Mkoa wa Ruvuma, katika kijiji cha Nahoro kilichopo Kata ya Luegu Wilaya ya Namtumbo.
Katika Operesheni hiyo iliyofanyika kwa kushirikiana na Askari wa TAWA Kanda ya Kusini, pia walifanikiwa kukamata watuhumiwa watatu Jafari Likwata (41), Nicodemus Pius Ngonyani, (60) na Jafary George Ngesela wakiwa na Nyara za Serikari Meno ya Tembo mazima 18 na vipande 11 waliyoyahifadhi kwenye mfuko na kuficha maeneo tofauti kwenye nyumba walizokuwa wananishi.
Aidha, katika kata ya Muhuwezi Tarafa ya Nakapanya Wilaya ya Tunduru kupitia Operesheni hizo walifanikiwa kukamata silaha mbili aina ya Rifle na Gobole na watuhumiwa Ally Rashidi Mbalamula (30), Amanzi Issa Wilium (25) na Mohamed Selemeni Omary (37), wakizimiliki kinyume cha sheria.
Pia katika Kijiji cha Muhukulu Wilaya Songea walifanikiwa kuokota Silaha moja aina ya Gobole iliyokutwa imetelekezwana watu wasiofahamika, katika Ofisi ya Kitongoji cha Chepukila Kijiji cha Muhukulu huku msako ukiendelea kuwasaka wahusika.
Aidha, Polisi pia walifanikiwa kukamata, jumla ya watuhumiwa 17 wakiwa na Pombe ya Moshi (Gongo) Lita 20, Pikipiki tatu (3) zenye namba za usajili MC.544 AUA aina ya SANLG rangi nyekundu, MC.955 CDD aina ya Houjue, MC.293 CCN, Engene moja aina ya Houjue, Mifuko minne ya Cement, Marumaru 48PC mali ambazo zidhaniwazo kuwa ni za wizi pamoja na watuhumiwa sita wakiwa na bangi kete 124, Mbegu za bangi 500 gm na Bangi kavu ikiwa imehifadhiwa.