Magwiji wawili ndani ya kikosi cha Azam FC chini ya Kocha Mkuu Yusuph Dabo wameibeba mechi ya Simba SC kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo aambao ni kiporo cha Mzunguuko wa Kwanza wa Ligi Kuu msimu huu 2023/24, tayari umeshapangiwa ratiba na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ‘TPLB’, ukitarajiwa kuchezwa Februari 09, 2024.

Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem lbwe amesema kuwa ni mchezo muhimu kwao na wanafurahi kwa kuwa wachezaji wao wataubeba vema kulingana na namba zao ambazo wanazivaa.

“Unaona mchezo wetu dhidi ya Simba SC unakuja, tarehe itakuwa ni namba ya Sopu, (Abdallah Suleiman) anayevaa jezi namba 9 huku ile nyingine ikiwa ni namba ya Akamiko (James) yeye huvaa namba 2 tupo tayari” amesema Ibwe.

Kwa sasa Azam FC ni vinara kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kucheza mechi 12 ilikusanya pointi 31, Simba SC ni nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23.

Zaidi ya 4,000 wapata maambukizi 'Red Eyes'
MAKALA: Ukipanda hekima unavuna heshima