Nanasi ni tunda zuri na kila mtu analipenda lakini hakuna watu wanaopenda Nanasi kama Wageorgia. Inaarifiwa kuwa katika karne ya 18, Mananasi yalifikishwa Nchini humo kutoka nje na ilikuwa ni gharama kubwa sana kuyanunua.
Hivyo, ni watu matajiri pekee walioweza kumudu ulaji wa tunda hilo na pia inadaiwa hata nguo walizovaa ikiwemo majoho walidarizi picha za mananasi kuonesha huba kwa tunda hilo.
Hata hivyo, wengine walienda mbali zaidi na hata wengine kutengeneza nyumba zao kwa kutumia mfano na rangi za Mananasi ambazo waweza kuziona hadi hii leo nchini humo.
Tumabie wewe ni tunda gani waweza chapisha katika nguo na ukajivalia mtaani kama majivuno kwa penzi zito ulilonalo kwake.