Klabu ya Singida Fountain Gate imemleta Kocha wa Makipa, Frank Peterson kutoka Denmark atakayeendesha programu za ‘Wadaka Mishale’ wa klabu hiyo na nje ya klabu ili kuwaibua, kuwaongezea uwezo na hata kuwauza baadae.

Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Kelvin Shabani amesema kocha huyo atakuwa pia na majukunu ya kulishauri benchi la ufundi la timu hiyo kutokana na uzoefu alionao.

“Singida tumekuwa tukikuza vipaji vya vijana na wanawake.Kwa kuangalia hilo tunaona tuingie ushirikiano na kocha Frank atusaidie sio tu Fountain, lakini hata jamii nzima kwa wanaohitaji,” amesema Shabani

Awali, Peterson alisema anafurahi kufanya kazi na Fountain na ataangalia baadhi ya makipa ambao watapata fursa ya kuwaendeleza nje.

Meneja wa kitengo cha uhusiano wa kimataifa wa klabu hiyo, Denis Joel amesema baada ya makubaliano hayo tayari kuna akademi mbili za Denmark wameingia nazo ushirikiano ili kuhakikisha wanapeleka vijana kujifunza soka nchini humo.

“Tunaangalia ni fursa gani anaweza kupata kijana katika taasisi yetu, hivyo kitengo cha kimataifa tayari kimepata (mtu) na huwa kila wanafunzi wa kidato cha nne na sita wanapohitimu wenye vipaji baadhi tunawaendeleza kwenye akademi za nje,” amesema Joel

Malimwengu: Hili sio penzi ni huba zito
Serikali yakamilisha usanifu Mradi wa Maji Kisarawe