Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ Paul Onuachu amewatahadharisha wachezaji wenzake kwa kuwataka wapambane kwa asilimia zote katika mchezo wa Robo Fainali ‘AFCON 2023’ dhidi ya Angola.

Nigeria itakua na kibarua cha kukabilia Angola kesho Ijumaa (Februari 02) katika Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, mchezo ambao utaanza majira ya saa mbili kwa saa za Afrika Mashariki.

Onuachu amesema ‘Super Eagles’ wanapaswa kuwa makini ili waweze kukabiliana na Angola, ambao wameonesha kiwango cha hali ya juu katika Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

“Ni mchezo ambao tunapaswa kuuchukua kwa uzito, kama tulivyofanya katika michezo iliyopita. Hakuna mchezo rahisi hapa, hakuna mpinzani rahisi, haswa linapokuja suala la kukabiliana na Nigeria,”

“Kila timu inataka kuonyesha kwamba inaweza kuifunga Nigeria, hasa zile ambazo hazipewi nafasi kubwa, lakini kwa Angola ya mwaka huu kila mmoja ameona uwezo wao, upo juu sana.

“Kila mtu anajua mchezo huu umekaa kimtego, lakini Nigeria tumejiandaa kukabiliana na Angola, kwa hivyo utakuwa mchezo mgumu. Lengo langu, lengo la timu, lengo la nchi ni kurejea Nigeria na kombe.” Onuachu amesema

MALIMWENGU: Wafanya sherehe kumtisha Shetani
Ujenzi Miundombinu Hospitali za Wilaya yagharimu bil.195.3