Taasisi ya Taifa ya Utawala Bora Nchini Ethiopia, imesema takribani watu 400 wanadaiwa kufa kwa njaa katika Mikoa ya Tigray na Amhara katika miezi ya hivi karibuni.
Tarifa hiyo, inakuja kufuatia Maafisa katika mikoa ya Tigray na Amhara kuripoti vifo vilivyotokana na njaa katika Wilaya za Mikoa hiyo, lakini Serikali ya shirikisho ya Ethiopia ikakanusha habari hizo.
Hata hivyo, Taasisi hiyo iliwafikisha Wataalamu katika mikoa hiyo iliyokumbwa na ukame na vita vilivyomalizika miezi 14 iliyopita na kugundua jumla ya watu 351 walikufa kwa njaa Mkoa wa Tigray na 44 katika Mkoa wa Amhara.
Aidha, inadaiwa kuwa ni asilimia 14 pekee ya watu milioni 3.2 waliolengwa kupatiwa msaada wa chakula na wa kibinadamu na mashirika ya Tigray, kati ya walipokea chakula hadi kufikia Januari 21, 2024.