Uongozi wa Tabora United umesema kikosi kinatarajia chao kutarejea mjini Tabora kesho Jumamosi (Februari 03) kikitokea Shinyanga kilipokuwa kimeweka kambi ya muda mfupi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi kuu msimu huu 2023/24.

Mhamasishaji wa klabu hiyo ya Tabora United, Pendo Lema amesema timu yao itakaporejea itaingia kambini moja kwa moja kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo unaofuata ambao wanatarajia kucheza na Simba SC katika uwanja wao wa nyumbani wa Ally Hassan Mwinyi.

Timu inarejea kesho Jumamosi ikitokea mkoani Shinyanga tulipoweka kambi kwa muda wote ambapo ligi iliposimama. Ikifika Tabora moja kwa moja itaingaia kambini kujiandaa na mchezo wetu unaokuja dhidi ya Simba SC.

“Shahuku ni kubwa sana kwa wachezaji tangu tukiwa kule Shinyanga vijana wetu wameonyesha nia ya kuutaka mchezo huu kwa hamu, hata mashabiki nao wamekuwa na kiu kubwa sana na mpaka sasa navyozungumza mashabiki kutokea maeneo mbalibali hapa Tabora wameshawasili mjini kuona timu yao pendwa ikifanya balaa siku ya Jumanne.

“Niwambie tuu kuwa wembe uliowanyoa wengine katika ligi ndiyo utakaokuja kumnyoa Simba siku ya Jumanne” amesema Lema.

Kevin de Bruyne: Liverpool mjipange
Mikel Arteta akubali kushindwa