Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne amewatisha wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England kuwa watapambana hadi mwisho kuhakikisha wanatetea taji lao.

Kiungo huyu wa kimataifa wa Ubelgiji, alianzishwa katika mechi yake ya kwanza kwa msimu huu juzi dhidi ya Burnley baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamuandama.

Tunafahamu kwamba tukipoteza tunazidi kujiweka mbali zaidi na ubingwa, inatakiwa tushinde tu, tukipoteza na Liverpool ikishinda inakuwa inatutupa mbali sana inatakiwa tuendelee kupambana na matumaini yangu kwamba tutaendelea kusalia kusogelea ubingwa na kupambana hadi dakika za mwisho.”

Kwenye mechi yake ya kwanza De Bruyne alitoa asisti ya bao la pili la Man City lililofungwa na Juelien Alvarez katika dakika ya 22.

Tabora United kuiwahi Simba SC

Baada ya mechi kocha wa Man City Pep Guardiola alimpongeza fundi huyu kutokana na kiwango alichoonyesha baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.

“Ulikuwa ni muda mrefu, miezi mitano hakuwa amecheza, amerudi akiwa na nguvu za kutosha, amecheza vizuri sana, nina matumaini makubwa kwamba yeye na Haaland wataenda kuisaidia sana timu kwenye hii hatua msimu huu.” alisema.

Ushindi huo uliwezesha Man City kufikisha pointi 46 ikiwa ni baada ya kucheza mechi 21, ikishinda 14, sare nne na kufungwa tatu.

Mbali ya kuibuka na ushindi, Guardiola alimpongeza kocha wa Burnley, Vincent Kompany ambaye ni kapteni wa zamani wa matajiri hao wa Jiji la Manchester kutokana na maendeleo yake na kusisitiza siku moja anaweza kwenda kuwa kocha wa Man City.

Ameshakuwa kocha mkubwa nina matumaini kwamba siku moja atakuwa hapa, ukiangalia timu yake jinsi inavyocheza na kuzuia, kiukweli napenda anachokifanya.”

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 3, 2024
Tabora United kuiwahi Simba SC