Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Moses Phiri amesema amerudi kwenye utawala wake kwenye ligi ya Zambia kilichobaki kwake ni kuonyesha alichonacho akiwa na Power Dynamos.
Phiri amejiunga na timu hiyo kwa mkopo wa miezi sita akitokea Simba SC kuchukua nafasi ya Thomas Chideu aliyetimkia Green Eagles FC.
Phiri ambaye aligoma kuzungumnzia chochote kuhusu Tanzania kwa madai kwamba ameshafunga hilo faili, amekiri kumalizana na timu hiyo huku akisisitiza kuwa bado ana uwezo wa kufanya vizuri na anaiona nafasi yake ndani ya timu hiyo atafanya kile kilichompeleka ikiwa ni pamoja na kujiweka kwenye ushindani.
“Ligi ya Zambia ni mwenyeji nayo nafahamu ushindani wao siingii kama mgeni kazi yangu ni kufanya kazi kwa kuhakikisha naonyesha utofauti na waliopo kwa kufanya kwa ukubwa,”
“Hilo linawezekana kwani bado naanmini nipo kwenye nafasi hiyo ya kufanya vizuri licha ya changamoto za hapa na pale lakini nina imani kubwa ya kufanya kitu ambacho kitarudisha jina langu kwenye washambuliaji wanaofanya vizuri.” amesema.
Mshambuliaji huyo akizungumzia maisha yake mapya kwenye timu hiyo amesema ana kazi kubwa ya kufanya kuwathibitishia waajiri wake hao wapya kwamba hawajakosea kumpa nafasi huku akisisitiza kuwa anaamini katika kujituma.
Tabora United kuiwahi Simba SC
Phiri ameondoka Simba SC msimu huu akiwa tayari amecheza dakika 278 kwenye mechi tisa ikiwa ni wastani wa dakika 31 kwa mchezo, huku akifunga mabao matatu tu.