Askari wa Kampuni Binafsi ya Ulinzi ya Ruhmwa ilioko Kata ya Matemanga Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wametakiwa kuhakikisha wanazingatia taratibu na sheria za Ulinzi pindi wapaokuwa wakitekeleza majukumu yao ili kuhakikisha wao na maeneo yao ya Ulinzi yanakuwa salama.
Hayo yamesemwa na Polisi Kata ya Jakika, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Robert Hatibu akiambatana na Koplo Charles wakati wakitoa elimu ya Ulinzi Shirikishi kwa askari wa Kampuni hiyo February 05, 2024.
Amesema, Askari hao wanatakiwa kuachana na tabia za ulevi pindi wawapo kazini sambamba na kuepuka kupokea vyakula toka kwa watu wasiowafahamu ili kuepuka kuwekewa dawa za kulevya kupitia vyakula hivyo na kusababisha maeneo yao ya malindo kuvunjwa na kuibiwa pamoja na wao kupoteza maisha yao.
Mkaguzi Hatibu pia alikemea walinzi hao kuacha tabia za kukaribisha watu kwenye malindo, yao kwani wengiwao hutumia njia hiyo kuwalaghai kuwa ni watu wema na baadae kuwadhuru kisha kuiba mali za watu katika malindo yao na kutokomea kusikojulika.