Kitendo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha, Polisi Kata wa Biro na Mtendaji wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Malinyi, kufika shule mbalimbali mara kwa mara kwa ajili ya kutoa elimu kimepelekea uwepo wa urafiki na wanafunzi wengi ambao wanafurahishwa na namna anavyowafundisha na kuwajali kama mwalimu Mlezi hivyo kuwafanya Wanafunzi wanaopita nje ya kituo cha Polisi wakati wa kurudi shule kumuulizia na kumsalimia.

Kati ya Wanafunzi hao, wapo Mapacha watatu ambao ni Elliah, Elisha na Ellison Sellesleus, Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Malinyi, ambao wamekuwa na mazoea ya kupita katika kituo cha Polisi Malinyi huku wakimuulizia Mkaguzi Rasha kwa lengo la kumuona na kumsalimia kabla ya kurudi nyumbani.

Mkaguzi Rasha amesema, kutembelewa na watoto hawa mapacha ni matokeo chanya ya elimu anayotoa mashuleni na kuwafanya wanafunzi wasiogope tena na badala yake kuwa karibu na Polisi na kuamini wapo sehemu salama.

Awali, ilizoeleka kuwa Wanafunzi au watoto wadogo kuwa na mazoea ya kuogopa Polisi au kituo cha Polisi kitendo ambacho kimepelekea Wazazi au walezi kutumia neno “Polisi” kuwatishia watoto wao, lakini kwa sasa imekuwa tofauti kwani Jeshi la Polisi kote nchini limekuwa likiweka urafiki na watoto, ili kuondoa dhana hiyo na kuwapa elimu inayowasaidia kujiamini na kuwa na uwezo wa kujieleza mbele ya Polisi iwapo watafanyiwa vitendo vya Ukatili.

Ushawishi wa Tanzania Duniani utategemea Ubora Sera Mambo ya Nje inayorekebishwa
Madeni hatarishi yanaleta msongo wa mawazo - Mallya