Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka nchini Cameroon ‘FECAFOOT’ limekataa kuafiki maamuzi ya kujiuzulu kwa Rais Samuel Eto’o ambayo aliyachukuwa jana Jumatatu (Februari 05).

Eto’o alichukuwa maamuzi ya kutangaza kujiuzulu, kufuatia tuhuma kadhaa kumuandama zikiwemo za upangaji matokeo na rushwa.

Juma lililopita, gazeti la The Athletic liliripoti kwamba liliona ujumbe wa WhatsApp, barua pepe, barua na rekodi za sauti ambazo zinadaiwa kuunga mkono shutuma mbali mbali, zikiwemo kupanga mechi, matumizi mabaya ya madaraka, vitisho vya kimwili, kuchochea vurugu na kueneza habari za uongo nchini Cameroon.

Kamati Kuu ya ‘FECAFOOT’ imetoa taarifa ya kukataa uamuzi wa Eto’o kwa kusisitiza bado ina Imani na kiongozi huyo, hivyo anapaswa kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

Taarifa ya Kamati Kuu imeeleza: “Mwisho wa majadiliano na mashauriano yaliyofuata, wajumbe wa kamati ya utendaji waliamua kudumisha majukumu yao ya sasa na hivyo kukataa kwa kauli moja kujiuzulu kwa rais na hivyo kufanya upya imani yao kwake ya kuendelea na moyo ule ule wa ujenzi na maendeleo ya soka la Cameroon.”

, viwango kama inavyotarajiwa katika mpango wake uliopitishwa na mkutano mkuu wa uchaguzi wa Desemba 11, 2021,” shirikisho hilo lilisema katika taarifa, likirejelea tarehe ambayo Eto’o alichukua kama rais.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo haikutaja maamuzi yuoyote dhidi ya Kocha wa Cameroon Rigobert Song, hivyo anaendelea na majukumu yake kama kawaida ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi.

Osinhem hatarini kuikosa Afrika Kusini
Askari waonywa kuacha ulevi, soga wakati wa lindo