Bondia wa maarufu wa Mkoani Morogoro, Twaha Kassim maarufu kwa jina la Twaha Kiduku amewasihi Wananchi kutunza na kuhifadhi vyanzo vya Maji, pamoja na kupanda miti.

Bondia Twaha aliyasema hayo mara baada ya kutembelewa nyumbani kwakwe na baadhi ya Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu na kuzungumza mambo mbalimbali juu ya shughuli shirikishi za utunzaji wa vyanzo vya Maji na Mazingira.

Kiduku ni moja kati ya Wadau wakubwa wa utunzaji na uhifadhi wa Rasilimali Maji.

Makala: Kesho ni fumbo wakati sahihi ni leo
Baresi: Tutatumia mbinu za Ihefu FC