Beki wa zamani wa Manchester City, Benjamin Mendy amepewa muda zaidi wa kulipa deni lake la kodi kiasi cha Pauni 800,000 na hivyo kukwepa sakata la kutangazwa mufilisi.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 kesi ya kubaka na kunyanyasa iliyokuwa ikimkabili, amepanga kuipiga bei nyumba yake.
Mwaka jana alifutiwa ilisikika mahakamani Mendy amepanga kuipiga bei nyumba yake ya huko Macclesfield, Cheshire na ameshusha bei kutoka Pauni 5 milioni hadi Pauni 3.8 milioni.
Mauzo ya nyumba hiyo yanapaswa kufanyika ndani ya wiki nane zijazo. Kingine ni Mendy amepanga kuwafungulia mashtaka Man City kwa kuacha kumlipa mishahara yake baada ya kushtakiwa kwa tuhuma za kubaka 2021.
Mendy alisafishwa na mahakama juu ya tuhuma hizo za kubaka na kufutiwa mashtaka.
Awali, Mendy alidaiwa kuiambia mahakama angelipa deni la HMRC, Pauni 20,000 kwa mwezi kupitia mishahara yake atakayolipwa kwenye klabu yake ya Lorient ya huko Ufaransa, lakini hajafanya hivyo.
Taarifa zinadai Mendy alipewa wiki 12 za kulipia nyumba hiyo, lakini amejiweka kwenye matatizo makubwa baada ya kushindwa kulipa kodi ya kila mwezi.