Klabu ya Manchester United inahita Pauni 40 hadi 50 Milioni ili kumuuza winga wao raia wa England, Jadon Sancho anayecheza kwa mkopo Borussia Dortmund.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna timu iliyoonyesha nia ya kutoa kiasi hicho cha pesa ili kumpata Sancho ambaye hivi karibuni hajawa kwenye kiwango chake.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund, Sebastian Kehl alipoulizwa juu ya uwezekano wa kumsainisha mkataba kudumu Sancho alisema ni jambo gumu sana kufanikisha hilo.

Licha ya kiwango chake kuonekana kimeshuka Man United bado haihitaji kumuuza kwa hasara na badala yake imeshikilia kiasi hicho cha pesa kwa timu zitakazohitaji saini yake.

Sancho ambaye alijiunga na Man United mwaka 2021 kwa Pauni 71 milioni analipwa Pauni 250,000 kwa wiki na ni changamoto kwa timu nyingine ambazo zitatakiwa ama kulipa nusu au karibu na mshahara huo na kuhofia kuingia gharama huku wakiwa hawaelewi kiwango chake.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 8, 2024
Majanga yamshika pabaya Mendy