Lydia Mollel – Morogoro.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa (MCC) CDE, Mohamed Ally Kawaida amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kutoka ofisini na kwenda Madukani kuhakikisha bei ya Sukari na kuwachukulia hatua wale wanaozidisha bei kwa manufaa yao binafsi.
Hayo yamejiri katika hafla ya kutimiza miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi – CCM, ambapo Mkoani Morogoro ilifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtawala na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa huo.
Katika hafla hiyo, CDE Kawaida amewakumbushaVijana kujitokeza kwa wingi katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na kushiriki katika maamuzi ya vyombo vya kiserikali.
“Sasa nataka niwakumbushe vijana kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi nusu ya wakazi wa Tanzania nzima ni vijana Wakitanzania , sasa lazima tutumie wingi wetu ,lazima tutumie hari yetu na lazima tutumie utayari wetu wakuona kwa namna gani tunashiriki katika maamuzi ya vyombo hivi vyakiserikali,” alisema Kawaida.