Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni mlezi wa CCM Kanda ya Ziwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kufunga kilele cha maadhimisho ya Miaka 47 ya Chama cha Mapinduzi hii leo February 4, 2024.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa Kagera, Hamim Mahmoud wakati akiongea na Vyombo vya Habari kusu kilele cha maadhimisho hayo.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi – CCM Mkoa wa Kagera, Hamim Mahmoud.

Amesema maadhimisho hayo yatafanyika Wilaya Muleba katika uwanja wa Fatma na yatahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali pamoja na Wananchi.

Aidha, Mahmoud pia ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Wanachama wa CCM na Wananchi kiujumla, kushiriki kilele hicho ambacho kinafikia tamati yake hii leo Februari 4, 2024.

Vijana wahimizwa uadilifu matumizi Mitandao ya Kijamii
Wizara yaikosha Kamati ushirikishaji Wananchi Miradi ya Maji