Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Kagera, Hamim Mahmoud amewataka Vijana Nchini kutumia kwa uadilifu Mitandao ya kijamii kwa kutangaza maendeleo yanayoendela kutekelezwa na Serikali.

Mahmoud ameyasema hayo wakati akiongea na Vyombo vya Habari kuhusu kilele cha maadhimisho ya miaka 47 ya Chama cha Mapinduzi – CCM, huku akiwasisitiza kuacha tabia ya kukashifu na mambo mengine yasiyofaa.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi – CCM Mkoa wa Kagera, Hamim Mahmoud.

Amesema, kwasasa Taifa linahitaji vijana waadilifu na wazalendo, ambao watasaodia katika kupambana na usongeshaji mblele wa gurudumu la maendeleo, hivyo kuinua uchumi wao na pato la Nchi.

Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake hii leo Februari 4, 2024 ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Rais wa Namibia Hage Geingob afariki Dunia
Majaliwa mgeni rasmi kilele miaka 47 ya CCM Kagera