Klabu ya Pyramids ya Ligi Kuu ya Misri imemtangaza rasmi Krunoslav Jurcic kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2013/24.

Uamuzi wa kumtangaza Kocha huyo kutoka nchini Croatia, umekuja kufuatia kuondoka kwa Kocha Jaime Pacheco, ambaye alishindwa kufikia malengo ya klabu hiyo, kufuatia Pyramids kushindwa kufurukuta mbele ya Al Masry kwa kufungwa 3-1 na kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi ya Misri.

Mtihani wa kwanza kwa Kocha Jucic unatarajiwa kuwa mwishoni mwa juma hili, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri, ambapo kikosi chake kitakabiliana dhidi ya ZED FC.

“Jurcic aliwasili Cairo jana kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kusaini mkataba, alifanya hivyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa klabu Mamdouh Eid na mkurugenzi wa uhamisho Amr Bassiousy,” Imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

“Kwa mara ya kwanza ataanza kazi yake leo ​mchana kwenye Uwanja wa Ulinzi wa Air kwa kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya ZED FC.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka miaka 54 amewahi kufanya kazi na klabu za Dinamo Zagreb (Croatia), NK Maribor (Slovenia), Adanaspor (Uturuki) na miamba ya Saudi Arabia Al-Nassr.

Matumizi mifumo ya TEHEMA yaiwezesha OSHA kupata taarifa muhimu
Wapewa somo ukusanyaji wa mapato, utatuzi migogoro