Lydia Mollel – Morogoro.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Morogoro, imeahirisha tena kesi ya jinai namba 889 ya Mwaka 2024, inayohusu kugushi nembo na kutengeneza kinywaji cha pombe kali.

Kesi hiyo ya jinai iliyoletwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza, imeahirishwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Morogoro, Theresia Kaniki kutokana  na Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, Robert Kasele kupata udhuru.

Kesi hiyo ya Jinai, inamhusisha mshitakiwa namba moja Makame Mohamed Ally na wenzake watano wanaodaiwa kukutwa wakitengeneza kinywaji hicho kinyume cha sheria.

Washitakiwa katika kesi hiyo kwa mara ya kwanza walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, Robert Kasele Januari 11, 2024 ambapo wote walikana mashitaka.

Watuhumiwa wote sita walikamatwa Desemba 28, 2023, katika eneo la Tushikamane Manispaa ya Morogoro wanakodaiwa kukutwa wakitengeneza kinyaji hicho chenye kilevi.

Watuhumiwa wote wapo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi februari 14, 2024 itakapokuja kusikilizwa kwa mara ya kwanza.

Makatibu Wakuu wakutana kujadili masuala ya Lishe
Max Gradel: Ninasikia wanachosema mashabiki