Jumanne Februari 13, 2024 mwili wa Hayati Lowasa unatarajiwa kuangwa na viongozi na wananchi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Jumatano Februari 14 mwili wa Hayati Lowasa utapelekwa katika Kanisa la KKKT Azania Front kwa ajili ya ibada takatifu na kuaga.

Alhamisi Februari 15 mwili wa Hayati Lowasa utasafirishwa hadi jijini Arusha ambapo viongozi na wananchi watapata fursa ya kuaga katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alifariki jana (Jumamosi, Februari 10, 2024) wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam na tangazo la kifo chake lilitolewa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango.

Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango akimfariji mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu marehemu Edward Lowassa , Mama Regina Lowassa mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo Masaki Jijini Dar es salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Abdulurhaman Kinana akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, katika msiba wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowasa nyumbani kwake Osyesterbay Jijini Dar es Salaam.

 

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akimfariji mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu marehemu Edward Lowassa ,Mama Regina Lowassa mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo Masaki Jijini Dar es salaam. Februari 11, 2024.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa wakati alipofika katika Makazi ya Familia Masaki Jijini Dar es salaam tarehe 11 Februari 2024. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 12, 2024
Mbowe akumbuka ushupavu wa Lowassa mpenda mabadiliko