Kocha wa Afrika Kusini, Hugo Broos amewapongeza wachezaji wake kwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zilizofikia tamnati jana Jumapili (Februari 11) nchini Ivory Coast.

Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ ilipata ushindi wa mikwaju ya Penati 6-5 mbele ya DR Congo baada ya timu hizo kumaliza kwa sare tasa dakika 120 za mchezo na kujihakikishia medali ya shaba.

Licha ya kikosi chake kupewa nafasi finyu, vijana hao wa Hugo Broos walionyesha kiwango bora katika Fainali hizo huku ikizitupa nje baadhi ya timu zilizotarajiwa kufanya vizuri.

Kocha huyo raia wa ubelgiji, amesema anajisikia fahari kwa wachezaji wake kwa namna walivyopambana katika mechi zote za mashindano hayo.

“Vijana wamefanya kazi nzuri. Wameonyesha mwitikio mkubwa. Walijitahidi kufanya walichoambiwa na nilielewa hilo lilikuwa gumu.

Walikuwa na moyo na kuhamasishana na katika hili unaona una wachezaji 23 ambao wanataka kitu kimoja ambacho ushindi,” amesema Broos.

Hii ni mara ya pili kwa Afrika Kusini kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Fainali za ‘AFCON’ baada ya kufanya hivyo pia mwaka 2000.

Hali hii isipokabiliwa kuna madhara makubwa - Zito
Kocha Ouma atuma salamu KMC FC