Mlipuko wa bomu katika kambi ya wakimbizi, umesababisha vifo vya watu watatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku Afrika Kusini ikiridhia kupeleka wanajeshi wake 2,900 katika eneo hilo.
Tukio hilo, linatokea kipindi ambacho mapigano makali baina ya vikosi vya serikali na waasi wa M23 yakiendelea, huku ikidaiwa kuwa vikosi vya Serikali na waasi wa M23 viliendeleza mapigano yao mchana wa Februari 12, katika eneo la Sake, lililopo upande wa Magharibi mwa mji mkuu wa Goma.
Mapigano hayo, yameendelea hadi jioni ya kuamkia hii leo Jumanne Februari 13, 2024 na kwamba shutuma zimeelekezwa kwa kundi la M23 kuishambulia kambi ya Zaina na kusababisha vifo vya watu wengine watano na wengine 15 kujeruhiwa.
Waziri wa Mawasiliano na Msemaji wa Serikali wa DRC, Patrick Muyaya kupitia mtandao wa X Wamelishutumu Jeshi la Rwanda kwa kuhusika na tukio hilo, huku maelfu ya raia wakiukimbia mji wa Sake, na Kundi la M23 linadai wa kuteka maeneo makubwa ya jimbo hilo tangu lilipotoka katika hali ya utulivu mwishoni mwa mwaka 2021.