Kamati ya Afya Msingi Mkoa – PHC, Mkoani Manyara imejadili taarifa ya maandalizi ya Kampeni ya kutoa Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Surua na Rubella, inayolenga kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo kwa kuongeza kinga kwa walengwa ambao ni watoto wote wenye umri wa uanzia miezi 9 hadi miezi 59 (Umri chini ya miaka 5).
Kikao hicho kilichofanyika hii leo Februari 14, 2024 Mkuu wa Wilaya Babati, Lazaro Twange akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga amewapongeza Watumishi wa sekta ya Afya kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia Wananchi katika maeneo ya tiba na kinga ya magonjwa mbalmbali.
Amesema, “awashukuru na kuwapongeza Wadau mbalimbali wanaoshirikiana na sisi katika kuboresha huduma za Afya za Afya, Mikoa mingi ukiwemo Mkoa wa Manyara na Halmashauri nyingi zimebainika kuwa na milipuko ya ugonjwa wa Surua na Rubella, ambapo kwa Mkoa wa Manyara jumla ya wagonjwa 601 walithibitika kuugua ugonjwa wa Surua na wawili walipoteza maisha.
Katika hatua nyingine, Twange amewataka wajumbe wa kikao hicho kuwa mabalozi wazuri wa kutoa taarifa sahihi kwa wananchi ili tarehe ya Kampeni itakapofika watoto wote husika wapelekwe kwenye vituo vya Chanjo kupata haki yao.
Aidha, Mkoa Manyara kuchanja jumla ya Watoto 313,284 kutoka katika Halmashauri zote 7, ambapo kwa Babati Wilaya wapo 65,145 Hanang Watoto 63,480, Mbulu Wilaya wapo 43,583, Simanjiro ni 42,218, Kiteto 57,435, Babati Mji 16,028 na Mbulu Mji 25,438.