Waumuni wa dini ya Kikristo wametakiwa kumrudia mwenyezi MUNGU na kuwa watu wa sala kwa kuongeza kasi asubuhi na jioni wakiwa Kanisani, Nyumbani hata kwenye jumuiya ndogo ndogo, ili kupata huruma ya MUNGU katika mfungo wa Kwaresma.
Akizungumza wakati wa ibada ya Jumatano ya majivu katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mama wa Huruma – Bukoba Askofu Mstaafu, Mhasham Method Kilaini amesema kipindi hiki Wakristo wanatakiwa kuwa karibu na MUNGU kwa kufunga na kuomba, ili waweze kupata mafanikio katika maisha yao.
Askofu Mstaafu, Mhasham Method Kilaini.
Hata hivyo, Askofu Kilaini ameendelea kuwasisitiza Wazazi na Walezi kuhimiza hasa kwenye mfungo wa kwa resima ndani ya siku 40,Watoto wao kusali na kuwa na maadili mema kwenye jamii inayowazunguka.