Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema namna bora ya kumuenzi Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa ni kuendelea kuyaishi maono yake ya uzalendo, uwajibikaji ili iwe dira ya kuzidi kujenga umoja na kupiga hatua za maendeleo nchini.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati alipokiwa akitoa salamu za pole na kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

  • Msiba huu si wa familia yetu pekee – Fred Lowassa

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia ametoa salamu za Pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na wananchi wote kwa msiba huo.

Hata hivyo, amesema amejifunza mengi kutoka kwa Hayati Edward Lowassa ukiwemo uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na watu wa makundi yote na kuweka mbele maslahi ya nchi.

Xavi Alonso aitisha Man Utd
Tanzania yatarajia kukuza uchumi kwa kasi Duniani - ILO