Huyu ni Harriet Tubman Mwanamama aliyekuwa ni Mwanaharakati wa kijamii wa nchini Marekani, anajulikana hata leo kama mpigania uhuru, jasiri na mkomeshaji wa mambo ya kitumwa. Baada ya kutoroka utumwani, Tubman alifanya misheni 13 za kuwaokoa takriban watu 70 waliokuwa watumwani ikiwa ni pamoja na familia yake na marafiki zake.

Harriet Tubman Alizaliwa utumwani huko Araminta Ross, akalelewa Pwani ya Mashariki ya jimbo la Maryland. Alipewa jina la “Harriet” na mama yake Harriet Ross. Jina la Tubman alilitoa kwa mume wake wa kwanza, John Tubman ambaye pia alikuwa ni mtu mweusi, aliyefunga naye ndoa mwaka 1844 kisha baadaye alilikimbilia jimbo huru la Pennsylvania kukwepa utumwa mwaka wa 1849.

Akiwa Pennsylvania, alikuwa akirejea Maryland kuwasaidia watu kutoroka utumwani, akitumia mbinu ya kubeba kuku. Mbinu hii aliitumia ili asitiliwe shaka, alikuwa akiwaachia kuku na kuwakamata tena. Vurugu za kuwakimbiza kuku ziliwakengeusha mabwana wa watumwa na hawakuweza kutambua yeye ni nani na kuna wakati pia alikuwa akijifanya anasoma gazeti, maana watu waliokuwa watumwa hawakutakiwa kusoma, hivyo wasingemshuku.

Kufuatia ufanikishaji wake wa uokozi, Harriet alipewa jina la utani la “Musa” akifananishwa na kisa cha Nabii Musa katika Biblia ambaye aliwaongoza watu wake kwa uhuru, katika safari zake zote “hakuwahi kupoteza abiria hata mmoja.” Hata hivyo Kazi yake hiyo ilikuwa tishio la mara kwa mara la uhuru na usalama wake yeye mwenyewe endapo angegundulika.

Hii ilitokana na na Wamiliki wa watumwa kutogundua mbinu zake na hivyo kupishana na hatari ya kukamatwa kwani Sheria ya Utumwa ya utoro ya 1850 ilikuwa hatari na ilitumiwa kila wakati, ikitoa adhabu kali kwa mtu yeyote ambaye angesaidia kutoroka kwa mtumwa.

Harriet alivaa kofia nyingi, alikuwa mtetezi hai wa haki ya wanawake na alifanya kazi pamoja na wanawake kama vile Susan Anthony na wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Harriet pia alifanya kazi katika Jeshi la Muungano kama mpishi, muuguzi na hata mpelelezi.

Wakati fulani, Harriet alipatwa na maumivu ya kichwa ya muda mrefu, na hii ilitokana na jeraha la kichwa alilopata akiwa kijana wakati akijaribu kumtetea mwenzake. Licha ya kuumia kwake lakini alipata maono ya nguvu ambayo alimuhusisha MUNGU ili aweze kujiongoza yeye na wenzake wote aliowakomboa kwenye safari nyingi za Kaskazini kupata uhuru.

Kabla ya kifo chake mwaka 1913, Harriet aliwaambia marafiki na familia, “Ninakwenda kuwaandalia mahali.” na alipofariki alizikwa kwa heshima za kijeshi katika makaburi ya Fort Hill huko New York na baadaye mwaka 2016, Idara ya Hazina ya Marekani ilitangaza kwamba uso wa Harriet Tubman utaonekana kwenye sarafu ya Dola 20 kama kumbukumbu ya mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

Wachezaji Ivory Coast wazawadiwa fedha, nyumba
Mohamed Salah amerudi kazini