Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limetangaza makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL2024),  hatua ambayo inatarajiwa kuanza Machi 8.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa katika vyanzo vya habari vya Shirikisho hilo, Ligi hiyo itachezwa katika vituo vinne vya Njombe, Pwani, Manyara, na Mwanza ambapo kila kituo kitakua na jumla ya timu saba (7) zitakazochezwa ligi ya mkondo mmoja.

 Taarifa hiyo imewatyaka viongozi wa timu zote shiriki kuhakikisha timu zao zinaripoti katika vituo Machi 5, tayari kwa kuanza kwa michuano hiyo Machi 08.

 KUNDI A: NJOMBE Hausing FC (Njombe), Tutes Hub (Ruvuma), Don Bosco (Iringa), Tukuyu Stars (Mbeya), Mkwajuni FC (Songwe), THB FC (Rukwa) na Polisi Katavi (Katavi).

 KUNDI B: PWANI Kiduli FC (Pwani), Black Six (Dar es Salaam), Red Angels (Lindi), Stand FC (Mtwara), Moro Kids (Morogoro), Gunners FC (Dodoma) na Singida Cluster (Singida)

 KUNDI C: MANYARA Reggae Boys (Manyara), Arusha City (Arusha), Kawele FC (Kilimanjaro), Veteran Middle Age (Tanga), Mabao FC (Shinyanga), Maswa FC (Simiyu) na Eagle SC (Dar es Salaam).

 KUNDI D: MWANZA Rock Solutions (Mwanza), Bweri FC (Mara), Bukombe Combine (Geita), Leo Tena (Kagera), Mambali Ushirikiano (Tabora), Kandahari FC (Kigoma) na Friends Rangers (Dar es Salaam).

Chama afichua siri ya ubingwa 2023/24
Picha: Matukio msibani Monduli kumpumzisha Lowassa