Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ikiongozwa na Mwenyekiti, Denis Londo leo Februari 19, 2024 imewasili Mkoani Morogoro kwa ziara ya kazi.

Katika ziara hiyo Kamati itakagua utekelezaji wa miradi ya Elimu inayosimamiwa na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST).

Aidha, katika ziara hiyo kwa upande wataalamu wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI wameongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI, Sospter Mtwale.

Katwila: Mtibwa Sugar haitashuka daraja
Sanga aishauri serikali AFCON 2027