Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kilichosababisha wakapoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu ni kikosi chake kukosa muunganiko, hali iliyomsaidia kutambua mapungufu yaliyopo kwenye kikosi chake.

Kocha huyo amesema watatumia mapungufu ya mchezo kujituma kuanzia uwanja wa mazoezi ili kufanya vizuri kwenye mechi zinazofuata za ligi.

“Tuna kikosi chenye wachezaji mchanganyiko wa zamani na wapya ambao tumewaongeza kwenye dirisha dogo, kifupi bado timu haijapata muunganiko mzuri ndio maana tukapoteza mchezo dhidi ya Ihefu,” amesema.

Kocha huyo amesema pamoja na matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mchezo uliopita, lakini anaamini Mtibwa Sugar haitashuka daraja.

Amesema hiyo ni kutokana na wingi wa mechi zilizosalia kabla msimu kumalizika lakini pia mikakati waliyokuwa nayo katika mzunguko huo wa mwisho.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo ligi hiyo, ikikusanya pointi nane katika michezo 15 iliyocheza msimu huu.

Sekta binafsi mdau wa uchumi, maendeleo - Dkt. Mwinyi
Kamati ya Bunge yakagua utekelezaji miradi ya Elimu