Kwa mujibu wa tovuti Football Insider, Chelsea inafuatilia kwa karibu kile kinachoendelea kwa Mshambuliaji wa FC Bayern Munich, Harry Kane ili kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hivi karibuni kocha wa Bayern, Thomas Tuchel alithibitisha kwamba staa huyo hana furaha kuendelea kusalia kwenye timu hiyo kutokana na kiwango ambacho imeonyesha tangu kuanza kwa msimu.

Chelsea inataka kumsajili Kane kwa sababu ina uhitaji mkubwa kwenye eneo hilo ambapo ilijaribu kufanya usajili katika dirisha lililopita, lakini haukukidhi mahitaji.

Uwezekano wa Chelsea kuipata saini ya Kane unaonekana kuwa mkubwa kwa sababu ya ukaribu uliopo baina ya kocha Mauricio Pochettino na staa huyo.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote na kufunga mabao 29.

Waanguka Mahakamani kwa kuishiwa nguvu
Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya yashika kasi