Kocha kutoka nchini Norway Ole Gunnar Solskjaer amezingatiwa kama chaguo la kujaza nafasi kama kocha wa muda pale Bayern Munich ikiwa Thomas Tuchel atafukuzwa, kwa mujibu wa Sky Sport.

Tuchel anakabiliwa na shinikizo kubwa pale ‘The Bavaria’ ambapo Bayern iko katika hatari ya msimu wa kwanza bila taji tangu 2011/12, kutokana na kufungwa mara tatu mfululizo.

Sky Sport imeeleza kwamba, Solskjaer kocha wa zamani wa Manchester United ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi kama Tuchel atafukuzwa, ingawa miamba hao wa Ujerumani bado wana nia ya kumweka bosi wao wa sasa katika nafasi ya kumpa nafasi ya kubadilisha mambo.

Solskjaer alishinda mechi 91 kati ya 168 akiwa kocha wa Man Utd, baada ya hapo awali kufurahia vipindi viwili vya kuinoa miamba ya Norway, Molde na Cardiff City.

Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern, Christoph Freund, anamfahamu Solskjaer vema na inasemekana amekuwa karibu naye sana kwa miaka mingi raia huyo wa Norway.

Pia kuna nia ya mchezaji wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane, ambaye alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu kama kocha Real Madrid.

Kufungwa kwa Bayer Leverkusen na Bochum kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’, kumeifanya Bayern kushuka kwa pointi nane nyuma, huku wakihitaji kupindua kipigo cha mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora na SSC Lazio baada ya matokeo duni na kusababisha sare 1-0.

Leverkusen kwa sasa inanolewa na Xabi Alonso, ambaye pia anatajwa kuwa shabaha ya Bayern.

Kitambi aikingia kifua Geita Gold
Jobe, Sarr wafichua kukata rasta