Wakazi wa mji wa Magugu uliopo Wilayani Babati Mkoani Manyara wameandamana na kufunga barabara kuu ya Babati Arusha na kuzuia abiria wanaoenda mikoa mbalimbali kukwama kwa zaidi ya saa nne sasa kutokana na tukio la mauaji.
Wananchi wanadai kusikitishwa na tukio la mauaji ya mtoto mdogo Maria Chacha (7), ambaye aliuawa kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwililiwili Februari 20 mwaka huu.
Wamesema, wanashinikiza kuachiliwa kwa anaedaniwa kuhusika na mauaji hayo i washughulike naye, ambae amekamatwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi kituo kidogo cha Magugu.