Wawakilishi wa mashirika ya kiraia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, wameonesha wasiwasi wao kuhusu ombwe la uongozi lililosababishwa na hatua ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na Mawaziri wengine Nchini humo.
Wajumbe hao wamesema hatua hiyo huenda ikatoa mwanya wa kuwapa nguvu waasi na kusambaa kwa machafuko zaidi katika maeneo mbalimbali Nchini humo.
Februari 20, Waziri Mkuu wa DRC, Jean-Michel Sama Lukonde Kyenge alipeleka barua ya kujiuzulu sambamba na Mawaziri kadhaa akiwemo Waziri wa Ulinzi kwa Rais Felix Tshisekedi katikati mwa machafuko ambayo yanazidi kuongezeka.
Hata hivyo, ujiuzulu kwa Kyenge kunafuatia uamuzi wake wa kubakia kuwa mbunge katika bunge la taifa.