Klabu za FC Barcelona na Atletico Madrid zinatarajia kuingia vitani kuipata huduma ya Mshambuliaji wa Manchester United, Mason Greenwood dirisha lijalo la majira ya kiangazi na Mashetani Wekundu inadaiwa kutaka kumuuza kwa kiasi kisichopungua Pauni 34 milioni.

Greenwood ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Getafe, msimu huu amefunga mabao matano na kutoa asisti tano kwenye mechi 21 za La Liga.

Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, Getafe ilikuwa inahitaji kuendelea kusalia na staa huyu kwa msimu ujao lakini inashindwa kufanikisha hilo kwa sababu ya mshahara wake wa Pauni 75, 000 kwa wiki.

Man United imepanga kuhakikisha inamuuza fundi huyu dirisha lijalo ili kuepuka kushuhudia akiondoka bure ifikapo mwakani.

Tangu kuanza kwa msimu huu fundi huyu amekuwa na mchangamo mkubwa katika kikosi cha Getafe. Mkataba wake na Man United unamalizika mwaka 2025.

Al Ahly yakwama Accra
Adel Amrouche amchefua Haji Manara