Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ustawi wa maisha hivi sasa umechangiwa na kazi kubwa na nzuri walioifanya Masheikh pamoja na Waalimu wa Dini waliotangulia mbele ya haki.

Dkt. Mwinyi amesema hayo katika Dua ya kuwaombea Mamufti, Masheikh, na Wanazuoni ambao walikuwa na mchango mkubwa Afrika waliotangulia mbele ya haki na baadae kuiombea baraka na amani Tanzania na Afrika kwa ujumla Dua iliyofanyika viwanja vya Msikiti Mkuu wa Bakwata (Mfalme Mohamed VI wa Morocco) jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mwinyi ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Samia, amesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano wa taifa katika kudumisha amani na kuendeleza mafundisho ya maadili na uadilifu hususani kuanzia ngazi ya familia na jamii yote.

Hata hivyo,ametoa shukrani kwa Bakwata kwa kuandaa na kuratibu Dua hiyo ya kuwaombea Wanazuoni Afrika.

NEC yatoa vibali utoaji elimu ya mpiga kura
Waliofariki ajali ya Lori Arusha wafikia 25